Anna Elisha Mghwira

Anna Elisha Mghwira (23 Januari 1959 - 22 Julai 2021[1]) alikuwa mwanasiasa wa Tanzania. Aliwahi kuwa mwenyekiti wa Alliance for Change and Transparency (ACT) aliyegombea urais wa nchi katika uchaguzi mkuu mnamo mwaka 2015.

Baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, alihamia chama cha CCM mnamo mwaka 2017.

  1. "Former Kilimanjaro RC Anna Mghwira dead at 62". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-07-23. Iliwekwa mnamo 2021-07-23.

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne